Sayyid Muhammad Rizvi
Asra Nomani ana maoni kwamba kule kutengana kwa wanaume na wanawake ndani ya misikiti kulianzishwa baadae kabisa katika historia ya Uislamu kuliko wakati wa Mtume (s.a.w.). Amejaribu pia kuliunganisha hilo na athar za Wahabi juu ya ulimwengu wa Kiislamu. Maoni hayo ni ama ujinga tu kwa upande wake au udanganyifu wa wazi wa kiakili.
Kutenganishwa kwa jinsia kunaonekana kwenye misikiti, kukiendeshwa na madhehebu zote za Kiislamu, kuanzia Sunni hadi Shi’ah, na Wahabi hadi Sufi, kwa misingi ya dhahiri iliyoachwa na Mtukufu Mtume wa mwisho. Utenganisho ni urahisishaji tu kuelekea kwenye staha, ambao unatumika kulingana na mazingira, kwa ajili ya kudumisha uingilianaji unaostahiki ambao ni kinyume uchanganyaji holela wa jinsia katika sehemu za kijamii.
Kizazi cha kwanza cha Waislamu katika Marekani kilianzisha vituo vyao vya Kiislamu kwa rasilimali haba, zilizofuata mfano wa miundo yao ya kitamaduni ambamo wanawake walipewa nafasi ndogo na duni. Vile vile wao hawakuwa wametambua changamoto za nchi yao ya asili, mpya. Wakati sasa umewadia wa vituo vingi vya kidini kubadilishwa ili kushughulikia mahitaji ya wakati wetu na mahala tulipo, na kufanywa vile vile kuwa rahisi kukubalika ki-wanawake.
Lakini katika kutafuta kwao vituo vinavyokubalika kwa watumiaji, Waislamu wasije wakaacha kuangalia kiini cha maadili yao ya Kiislamu vile vile. Kituo cha Kiislamu kisiwe kinaakisi ile Sura yake ya kiusanifu majengo ya kipekee kwa nje tu, ni lazima pia iingize athari za maadili – unyofu wa Kiislamu kwenye jumuiya ya watu. Waislamu hawapaswi kuigiza kwa kuona aibu tu, kila kawaida ambayo wanaiona karibu yao, hususan pale uigizaji huo unapopingana na mafundisho ya Kiislamu wanayotangaza kuyafuata.
Uislamu umeegama juu ya Qur’ani Tukufu na Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.). Wakati ukiwa haulazimiki kuzikataa desturi za jamii za watu za kawaida, bado hauwategemei wale wafuasi wake kubadili kila ambacho kiko kinyume na maadili yake. Moja ya maadili ya msingi ya Kiislamu ni staha katika maingiliano baina ya jinsia.
Kile kisa cha Nabii Musa (a.s.) na wale mabinti wa Nabii Shu’aib (a.s.), kilichotajwa ndani ya Qur’ani Tukufu (28: 23 – 28) na hadithi, zinatukumbusha sisi juu ya staha ya nje na ya ndani (haya’a). Pale Musa alipokimbilia Misri na akafika Madayini, alifika kwenye kisima cha maji ambapo alikuta kundi la wanaume wachota maji kwa ajili ya mifugo yao. Hapo karibu yake, aliwaona vijana wawili wanawake wakiirudisha nyuma mifugo yao.
Aliwaendea wale wanawake wawili na akawauliza; “Ninyi mna matatizo gani kiasi kwamba mnalizidisha nyuma kundi la wanyama wenu?” binti hao wakasema: “Sisi hatuwezi kuchota maji mpaka wale wachungaji waondoke wao pamoja na kondoo wao pale kwenye kisima, na baba yetu ni mzee sana,” ikimaanisha kwamba asingeweza kuifanya mwenyewe kazi hiyo.
Baada ya kuitambua ile staha waliokuwa nayo wanawake wale ambao hawakutaka kuchanganyika na wanaume wageni, Musa alijitolea kuwasaidia. Akawanywesha wale kondoo wao kwa niaba yao, na halafu yeye akarudi kule kwenye kivuli kwa ajili ya kupumzika.
Baada ya kufika nyumbani kwao, wale madada wawili wakasimulia kile kisa chote kwa baba yao Shu’aib, ambaye aliwatuma wao kwenda kumwita Musa ili aweze yeye kumtolea shukrani zake kwake.
Halafu mmoja wa wale wanawake akaja kwa Musa akitembea kwa staha na akamkaribisha yeye kwa niaba ya baba yake. Wakarudi wote mpaka nyumbani kwa yule msichana huku Musa akitembea mbele ya msichana huyo ili asiweze kuona maungo ya mwili wake.
Baada ya Shu’aibu kumshukuru Musa, mmoja wa wale wasichana akasema: “Ewe baba yangu, kwa vile hatuna kijana wa kiume katika familia yetu, basi muajiri huyu ili akufanyie kazi; kwa hakika mtu bora ambaye waweza kumuajiri ni yule ambaye anazo nguvu na ni muaminifu.” Shu’aib sio tu alimuahidi kumuajiri Musa, bali alimfanya kuwa mkwe wake.
Kisa hiki cha Qur’ani Tukufu kinatufundisha sisi kwamba katika Uislamu : 1. Kujiingiza na kuchanganyika kwa wanawake na wanaume ambao hawana uhusiano kunapingwa na kukatazwa vile vile; 2. Wanawake wanaweza, wakati wowote inapokuwa ni muhimu, kushiriki katika nyanja za kijamii – Kisiasa – na kiuchumi za jamii nje ya nyumba zao, lakini pia ni lazima kwao kuyafanya hayo kwa haya’ (staha); 3. Hata katika maingiliano yanayoruhusiwa, haya’ (staha) ni lazima izingatiwe katika shughuli na jinsia tofauti; 4. Miongozo ya Kiislamu kuhusiana na utenganishi au kudumisha mipaka baina ya jinsia, hayo hayapo katika masuala ya Msikitini tu.
Idadi kubwa ya wanazuoni wengi wa Kiislamu, Sunni na Shia’h, wanazikubali desturi zifuatazo za Mtukufu Mtume (s.a.w.). Tunaona kwamba hata pale wanawake walipokuja wakiwa katika hijabu (vazi la Kiislamu) kuja msikitini kwa ajili ya Swala, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipendelea kwamba katika ule wakati wa kutoka msikitini, wanaume wabakie nyuma ili kwamba hao wanawake waweze wao kuondoka mwanzoni kwanza. Baadaye, katika wakati wa uhai wake bado, mlango tofauti wa kuingilia ulitengenezwa kwa ajili ya wanawake ili kuwezesha pasiwepo na fursa ya kuchanganyika humo ndani. Mtume (s.a.w.) vile vile hakuupenda ule mchanganyiko wa wanaume na wanawake ndani ya mitaa na barabarani. Hata pale wanawake waliposhiriki kwenye swala ndani ya msikiti, hao wanaume na wanawake hawakuchanganyika; wakidumisha umbali wao kimipaka. Hii kwa kiasi fulani ndio sababu kwa nini baadhi ya wanawake walimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.) kuweka siku maalum kwa ajili ya “wanawake tu,” ili kwamba wao waweze kukutana naye na kumuuliza maswali wakiwa mbali na wanaume.
Kwa hiyo kanuni katika jamii nyingi za Kiislamu imekuwa siku zote ni kuwaweka wanaume na wanawake mbali mbali kwa kizuizi au sehemu tofauti zilizodhihirishwa wakati wowote ule panapokuwa na mkusanyiko wa Waislamu. Ni wazi kwamba kawaida hii inaweza kufatiliwa kurudi nyuma kupitia karne na karne mpaka kwenye mfano wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) mwenyewe.
Dhana ya ‘haya’ (staha ya nje na ndani), inadhihirishwa katika mafunzo ya Uislamu katika namna na njia nyingine tofauti : Maingiliano ya kiheshima baina ya wanaume na wanawake, mfumo wa utaratibu wa mavazi, na vile vile utenganishaji wa jinsia katika mikusanyiko ya Kiislamu. Mtu anaweza pia kurejea kwenye Sura ya 24, Ayah ya 33 ya Qur’ani Tukufu kwa ajili ya mifano juu ya ni vipi wanaume na wanawake wanavyopaswa kutendeana, mmoja wao na mwingine.
Matokeo ya wazi ya kupuuza maadili ya ‘haya’ (staha) katika jamii ni kuongezeka kwa mambo ya kabla na ya ziada – yahusikanayo na ndoa, kuvunjika kwa ndoa nyingi na watoto kuzaliwa nje ya ndoa. Hii ni pamoja na kutosema lolote, kwa kweli, kuhusu kutamba kwa tabia ya kuaibisha kunakofanywa kwa kuzungumza bila haya juu ya mahusiano haramu ya kijinsia ya mtu – kitu ambacho kimekuwa sio hoja kwa baadhi ya watu.
Utenganishaji wa jinsia katika hadhara hakuhusiani na ubora au uduni wa mmoja juu ya mwingine, na kabisa huo sio “ubaguzi”. Utenganishaji wa jinsia unahusika na kujenga mwenendo mwema na staha. Kuwatenganisha wanaume na wanawake au kutilia nguvu staha katika mahusiano yao pia kunawasaidia wao kulenga kuwa macho kwenye kazi zao. Hiyo ni sababu mojawapo ya mashirika mengi yenye mafanikio kuwawekea vikwazo watumishi wao kutokana kuwa na mahusiano ya kimapenzi kati yao.
Inapokuja kwa mwanamke kujiingiza na kujihusisha kwenye jamii, kwa kweli Uislamu unaruhusu mahusiano ya heshima na yaliyotakasika. Kwa dhahiri kabisa hauruhusu, na unakataza hasa, uchanganyikaji usio na lazima wala umuhimu. Mtu anaweza akafanya uamuzi binafsi wa kutoufuata huu muongozo wa dhahiri, lakini basi mtu asije akategemea kwamba ati Uislamu uidhinishe au kuunga mkono tabia kama hiyo.
Mimi ninazifahamu taasisi au mashirika mengi ambamo licha ya utenganishaji wa kimaumbile katika vituo, wanawake wanashiriki kikamilifu katika ngazi zote za utoaji maamuzi na hatua zake. Kwa kweli, vituo vingi zaidi na zaidi vinahitajika kufanya hivyo, lakini kwa masharti ya Kiislamu, na wala sio yale ya kidunia. Sio Uislamu unaohitaji marekebisho; ni Waislamu ndio ambao wanahitaji kurekebishwa, ili kufikia daraja za juu katika unyenyekevu na utii kwenye utashi wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.).
Waislamu wanawake na wanaume wasiwe wenye kushindana dhidi ya kila mmoja wao; wanapaswa wawe wenye kushamirishana wenyewe kwa wenyewe katika kuendeleza yaliyo mema na kukatazana maovu (Qur’ani; 9:71).
Lakini je, hao wanaoitwa “Waislamu wenye kupendelea maendeleo” wanajua angalau nini.