Ni kuamini ya kuwa mwenyezi mungu ni mmoja hana mshirika, na wala hana mfano, wala hakuna anaefanana nae, hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hana umbile, ni mwenye kusifika na sifa za ukamilifu na ni mwenye kuepukana na sifa za upungufu, ni muumba wa ulimwengu na vyote vilivyomo.