3. UTUME:

Ni kuamini ya kuwa Mwenyezi Mungu mwenye hekima aliwachagua watu wema ili kuwaongoza viumbe na kuwaelekeza, na kuwabebesha ujumbe wake waufikishe kwa watu wote, na watu hawa ni manabii na mitume, mitume ambao kupitia kwao iliteremka rehma ya muongozo na uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuja kwa viumbe wake na idadi yao ilikua ni 124,000, wa kwanza wao ni Adam (a.s) na wa mwisho wao ni mtume Mohammad (S.A.W).