Ni kuamini ya kuwa uadilifu ni sifa moja wapo kati ya sifa za Mwenyezi Mungu iliyo nzuri. Na imani
hii inatokana na qur'an kutomnasibisha Mwenyezi Mungu na aina yoyote ya
dhulma. Kwani Mwenyezi Mungu anasema(( Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu
chochote hata kama ni uzito wa tembe moja)).
Na katika aya nyingine amesema ya kuwa;(( Mwenyezi Mungu amesimama juu ya
uadilifu)), pamoja na aya hizo hata akili inahukumu kuwa Mwenyezi Mungu ni
muadilifu kwa sababu ni sifa ya ukamilifu, na dhulma ni sifa ya upungufu na
akili inahukumu ya kuwa Mwenyezi Mungu alie takasika ni mwenye kusifika na sifa zote za ukamilifu, na ni mwenye
kutakasika na aibu ya aina yoyote na upungufu wa aina yoyote katika dhati
yake.