Sala ni moja wapo kati ya nguzo ambazo uislam umesimama juu yake, sala ikikubaliwa matendo mengine nayo hukubaliwa.Na sala za wajibu katika zama hizi ni tano:
(1). Sala tano za kila siku pamoja na sala ya ijumaa.
(2). Sala ya ayaat (alama ijitokezayo kama kushikwa kwa mwezi na kupatwa kwa jua, au kutokea tetemeko na alama zingine.
(3). Sala ya twawafu ya wajib.
(4). Sala iliyo wajibika kwa kuchukua malipo, sala ya nadhiri,sala ya ahadi, na sala ya kiapo na mfano wa hizo.
(5). Kumsalia maiti, pia huongezwa sala iliyompita mzazi wa kiume. Ihtiyati ya wajibu inamtaka mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu amlipie mzazi wake sala hiyo. [endelea]