Asili yake ni kuwa ni moja wapo kati ya faradhi zilizo sisitizwa na yenye kutolewa dalili katika qur’an na zimepokelewa riwaya nyingi zenye kutilia umuhimu, faradhi hii kutoka kwa Ahlul-baiti (A.S), na kati ya riwaya hizo baadhi zikiwalaani wenye kuzuwia kutoa khumsi na zingine zikimlaani mwenye kuitumia hali ya kuwa hastahili au kinyume cha sheria.