HISTORIA  FUPI YA IMAM ALLY  BIN  MUSSA RIDHAA (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YAKE  (A.S).

Jina lake tukufu ni  Ally bin Mussa bin Jaafar bin Mohammad bin Ally bin Hussein bin Ally bin  Abii twalib (a.s).

MAMA  YAKE  (A.S).

Mama yake alikuwa ni mjakazi alie kuwa akiitwa: Najmah, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

KUNIA YAKE  (A.S).

1- Abuul Hassan.  2- Abuu Ally, na mengineyo.

MAJINA YAKE MASHUHURI  (A.S).

1- Ridhaa. 2- Asswabir.  3- Arradhiyyu.  4-  Al wafiyyu.  5-  Al faadhil, na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE  (A.S).

Alizaliwa  tarehe  11 mwezi wa dhil qaadah, mwaka 148 hijiria, na kuna kauli zingine kuhusiana na tarehe ya kuzaliwa kwake  (a.s).

SEHEMU  ALIPO ZALIWA  (A.S).

Alizaliwa katika mji wa Madinatul munawwarah.

WAKEZE  (A.S).

1- Alikuwa ni mjakazi kwa jina  Sukainah  Marsiyyah, na inasemekana kuwa jina lake ni Khaziiraan.

2- Ummu Habiib binti Ma’amuun, na kuna jina lingine tofauti na hilo.

WATOTO WAKE (A.S).

1- Imam Mohammad Jawaad (a.s). 2- Al qaaniu.  3-  Jaafar.   4- Ibraahim.  5- Hassan, na inasemekana kuwa ana jina lingine tofauti na hilo.

NEMBO YA PETE YAKE (A.S).

Pete yake ilikuwa na nembo ifuatayo: (Maa shaa’allah, laa quwwata illa billahi).

UMRI WAKE  (A.S).

Ali ishi kwa muda wa miaka 55, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

MUDA WA UIMAMU WAKE  (A.S).

Uimamu wake ulidumu kwa muda wa miaka 20, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.  

WATAWALA WA ZAMA ZAKE (A.S).

1-Haruuna Rashiidi.  2- Amiin.  3- Maamuun.

TAREHE YA KUFA KWAKE  SHAHIDI (A.S).

Alikufa shahidi mwishoni mwa mwezi wa Safar, mwaka 203 hijiria, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

SEHEMU ALIPO FIA  SHAHIDI (A.S).

Ali kufa  shahidi katika Ardhi ya Tuus, katika mkoa wa  khorasaan kwenye mji wa  (Mash’had)   nchini Iran.

SABABU YA KUFA KWAKE  SHAHIDI  (A.S).

Ali uwawa shahidi kwa kulishwa sumu katika zama za mtawala  wa  kibani  Abbas  aliekuwa   akiitwa Maamuun.

SEHEMU ALIPO ZIKIWA  (A.S).

Alizikiwa  katika kijiji cha  Sanabaad  kilichoko  sehemu iitwayo Tuus (mkoa wa Khorasaan) nchini Iran.