HISTORIA  FUPI  YA IMAM MUSSA KADHIM  (A.S)

JINA LAKE NA NASABU YAKE (A.S).

Jina lake ni Mussa bin Jaafar bin Mohammad  bin Ally bin Hussein bin Ally bin abii twalib  (a.s).

MAMA YAKE  (A.S).

Mama  yake ni kijakazi  alie kuwa  akiitwa: Hamidah, na kuna kauli nyingine tofauti na hiyo.

  

KUNIA  YAKE  (A.S).

1- Abul Hassan.  2- Abu Ibraahiim. 3-  Abuu Ally.  4-  Abuu Ismaail na mengineyo.

MAJINA YAKE MASHUHURI (A.S).

1- Kaadhim.  2-  Abdusswaleh. 3-  Asswaabir.  4-  Al amiin na mengineyo.

TAREHE YA KUZALIWA KWAKE (A.S).

Alizaliwa  tarehe 7 mwezi wa safar  mwaka 128 hijiria.

SEHEMU ALIPO ZALIWA (A.S).

Alizaliwa katika sehemu iitwayo  (Abuwaa), katika mji wa Madinatul munawwarah.

WAKEZE  (A.S).

Wakeze wote walikuwa ni vijakazi.

WATOTO WAKE (A.S).

Takriban Imam alikuwa  na watoto  37: 1- Imam Ally bin Mussa Ridhaa  (a.s).  2- Ibrahiim.

3-  Abbas.  4- Qaasim.  5-  Ismaail.  6- Jaafar.  7-  Haarun.  8-  Hassan.   9-  Ahmad.

10-  Mohammad.  11-  Hamza.   12-  Abdallah.   13-  Is’haaq.  14-  Ubaidullah.  15-  Zaid. 16- Hassan.  17- Al fadhlu.  18-  Sulaimaan.  19- Fatimatul  kubraa. 20- Fatimatu sughraa. 

Ruqayyah.  22- Hakiimah. 23- Ummu abiiha.  24- Ruqayyah Assughraa.  25- Kulthuum. 26- Ummu Jaafar.  27- Lubaabah. 28- Zainab. 29- Khadijah. 30- Ulayyah.  31- Aaminah. 32- Hasnah. 33- Burayha.

NEMBO YA PETE YAKE (A.S).

Pete yake ilikuwa na  nembo ifuatayo: ( Hasbiya llahu), na kuna riwaya zingine tofauti na hiyo zizungumziazo  nembo yake.

UMRI WAKE  (A.S).

Aliishi kwa muda wa miaka 55.

MUDA WA UIMAMU WAKE  (A.S).

Uimamu wake  ulidumu kwa muda wa miaka 35.

WATAWALA WA  ZAMA ZAKE (A.S).

1- Abuu jaafar Mansuur Dawaniiqiy.  2- Mohammad  Mahdiy.  3- Mussa Al haadiy.  4- Haarun Rashiid.

TAREHE YA KUFA KWAKE SHAHIDI (A.S).

Alikufa  shahidi tarehe  25 mwezi wa Rajab, mwaka 183 hijiria, na kuna riwaya zingine zilizo taja    tarehe  tofauti na hiyo.

SEHEMU ALIPO FIA SHAHIDI  (A.S).

Alikufa shahidi  katika mji wa Baghdaad  huko nchini Iraq.

SABABU YA KUFA KWAKE  SHAHIDI (A.S).

Ali uwawa kwa kulishwa sumu katika zama za khalifa wa bani Abbas  aitwae Haruun Rashiid.

SEHEMU ALIPO  ZIKIWA (A.S).

Alizikiwa kwenye  makaburi ya maquraishi  katika mji wa kaadhimiyyah, kaskazini mwa mji wa Baghdaad.