KIONGOZI WA JUU WA KIDINI AYATULLAH AL-UDHMA ASSAYYID ALLY SISTANI.

UTANGULIZI.

Hakika mimbari ya imamu Khui (mungu amrehemu) iliyo dumu kwa muda wa nusu karne takriban alitoa matunda mema,na mazuri na ndio matunda bora zaidi na faida nzuri zaidi aliyo upatia umma katika uwanja wa fikra za kiislam,na katika elimu tofauti na mambo tofauti pia misimamo ya kiislam iliyo muhimu, kwani maulamaa mamia kwa maelfu na mamujtahi na wanazuoni wengi wenye fadhilo walio hitimu masomo yao kwake na ambao walibeba jukumu la kuendeleza mwendo wake wa kifikra na njia yake, njia aliyo jawa na utoaji wa elimu na fikra na kujitolea kwa ajili ya kuutumikia uislam na elimu na jamii, na wengi wao katika siku hazi ni walimu wa hawza mbali mbali za kielimu hasa katika mji wa Najaf tukufu huko Iraq na Qumit muqadassah ulioko Iran na miongoni mwao kuna waliofikia kiwango cha juu kielimu na kustahili au kuwa na uwezo wa juu kielimu na kijamii uwezo ambao unawapa nafasi na maandalizi ya kuwafanya waweze kusimamia jukumu la malezi na ufundishaji,na kuweza kubeba jukumu la marjiu (kuwa marejeo ya watu katika masuala ya dini) na jukumu katika uongozi katika zama hizi.
Na alie muhimu na alie dhihiri na kujitokeza zaidi kati ya mashupavu hao katika elimu, ni sayyid ustaadhi ayatullah al-udhma Assayyid Ally Al-hussain Asistaani.(mwenyezi mungu amuhifadhi) yeye ni mmoja wapo kati ya wanafunzi walio jitokeza na kudhihiri zaidi wa imam Khui, (Mungu amrehem) alie na kiwapa zaidi na mwenye elimu na mwenye fadhila na mwenye maandalizi au aliestahili kuwa kiondozi, na katika mistari hii michache mazungumzo yetu yata husiana na shakhsia ya mwanazuoni huyu mkubwa na tutaifupisha katika nukta zifuatazo.

KUZALIWA KWAKE NA MALEZI YAKE.
Sayyid alizaliwa tarehe 11/mwezi wa shaaban mwaka 1350 hijriaya katika mji mtukufu wa mash-had, katika familia ya kielimu na yenye kushikamana na dini,na alisoma masomo yake ya Ibtidaiya (ya mwanzo)na mukiddimati na satuhu,na akamaliza kwa kusoma masomo ya kiakili (kama mantiki na falsafa) kwa mashekhe wake na walimu wake hadi kuhitimu vema katika masomo ya Bahdhul-khariji katika mji wa mash-had na muhakiki mirzaa mahdi Al-isfahanuy (mungu amrehemu.)
Kisha akahamia kwenye hawzo au chuo cha kielimu kilichoko kwenye mji mtukufu wa Qum katika zama za marjui mkubwa Sayyid Hussein Burujardiy (mungu amrehemu) mwaka 1367, na aliudhuria kwenye masomo ya wana zuoni na maulamaa wakubwa kwa wakati huu, kati yao ni sayyid Burujudiy( mungu amrehemu) alihudhuria somo lake la fighi na USULU,na alifaidika sana na ujuzi wake wa kifighi na hadithi,kama amhavyo alihudhuria masomo ya fighi kwa mwanazuoni mwenye fadhila sayyid Al-hujja kuh-hakmariy (mungu amrehemu) na wanazuoni wengine wengi katika zama zake.
Kasha akauhama mji wa Qum na kuelekea kwenye hazina ya elimu na fadhila kwenye chuo cha kielimu katika mji wa Najafil-ash-raf mwaka 1371 4.
Na kuhudhuria masomo ya vigogo wa elimu na fikra wa zama hizo,kama ikam Al-hakiim na shekh Hussein al-hiliy na imamu khuiy radhi za mwenyezi mungu ziwe juu yao wote.
Na sayyid alibakia akihudhuria masomo ya imamu khuiy, kama fiqhi na Usul zaidi ya miaka kumi, kama ambavyo aliendelea kuhudhuria dauru kamili la somo la usul kwa shekh Al-hiliy. pia sayyid alijishughulisha na kazi ya utafiti na usomeshaji kwa kutoa mihadhara yaake (Bahthul-khariji) mwaka 1381 H. katika maudhui ya fiqhi kufuatana na kitabu Al-makaasibu cha shekh Al-answary (mungu amrehemu) na akamalizia kwa kukitolea maelezo kitabu Al-urwatul wuthqaa cha sayyid na faqihi. Twabatwabaiy mungu amrehemu, na katika kitabu hicho alikamilisha sherehe ya kitabu Atwaharo na sehemu kubwa ya matawi ya vifungu vya kitabu Aswala na sehemu ya kitabul-khumsi kama ambavyo alianza kutoa mihadhara yake (katika bahthul khariji) kuhusiana na usul katika mwezi mtukufu wa shabaani mwaka 1384.H, na alikamilisha daura lake la tatu la mihadhara katika mwezi mtukufu wa shaban mwaka 1411 H na wanafunzi wake walifanikiwa kuandika na kusajili mihadhara yake ihusianayo na fiqhi na usulu kwenye ripoti zao ambazo ni nyingi.

KUFIKIA KWAKE KUWA MARJIU.
Walimu wengi na wanazuoni wengi wenye fadhila wa Najaf wamenukulu ya kwamba baada ya kufariki ayatullah Assayyid Nasrullah mustanbat (mungu amrehemu) maulama kadha walitoa pendekezo lao kwa imamu khuiy (mungu amrehemu) kuandaa mazingira bora kwa mtu aashiriwae kwa vidole,na kumuandaa kwa ajili ya kuhifadhi na kulinda na fasi ya marjiu katika dini na kwa ajili ya kulinda hawza za kielimu katika mji wa Najaf, na chaguo lilimuangukia sayyid sistani (mungu amrehemu) kutokana na elimu yake bora, na kutokana na usafi wa mwenedo wake na tabia zake, na baada ya kufariki imamu khuiy (mungu amrehemu) sayyid alikuwa ni miongoni mwa watu sita walio lisindikiza jeneza lake usiku nae ndie alie usalia mwili wake uliatwahara, na baada ya hapo alichukua nafasi ya kuwa marjiu.
Na kufanyiwa taklit (kufuatwa kwenye mas-ala ya fiqhi) na uongozi wa hawza za elimu, kwa kutuma ijaza (ruhusu) na kugawa haki mbalimbali na kufundisha kwa kuitumia mimbari ya imam khui (mungu amuwie radhi) katika msikiti uitwao masjidul-hadhraau.
Na taklidi yake ikkanza kusambaa na kuenea kwa kasi katika Iraq na bara arabu na sehemu zingine kama India, Afrika na sehemu zingine na hasa kati ya waheshimiwa kwenye hawza za kielimu, na makundi mengine tofauti kati ya watu wenye elimu na vijana. Kutokana na kuwa na fikra za kiwango cha juu na zilizo endelea za kitamaduni, na sayyid mwenyezi mungu amlinde ni miongoni mwa maulamaa wachache wafiqhi ambao wanasifa ya (Aalamiya) kuwa na elimu zaidi kuliko wengine kwa ushahidi wa maukamaa kadhaa na walimu kadhaa wa hawza ya kielimu wa Najaf na Qum, na tunamuomba mwenyezi mungu akidumishe kivuli chake kilicho kipana juu ya waja na amfayie kuwa ni akiba yetu na kimbilio letu.

VITABU VYAKE.
Tangu akiwa na umri wa miaka 34,alianza kufundisha badhthul-khaarriji katika madda ya fiqhi, na usulu na il-murrijaal, na akitoa nadharia zake na fikra zake ambazo ni nyingi, na alifanya bahthi ya makaasib, Twahara swala,kadhaa, khumsi na baadhi ya kanuni za kifiqhi kama riba na kanuni ya takia, na kanuni ya ilzaam.
Na alifundisha usul-duru tatu na baadhi ya bahthi hizi zimekwisha andaliwa kwa ajili ya chapa kama bahthi zake za usul-ilimiyya na taadul- na tarjiih, pamoja na bahthi zingine za kifiqhi na baadhi ya milango ya sala na kanuni ya takia na il-zaam.
Na kuna maulamaa wengi wakubwa walio chipukia kutokana na bahthi zake, na baadhi yao wamefikia katika kiwango cha kufundisha bahthul khariji, kama allama shekh Maheliy Mar'wariid na al-allamh ssayyid Habiib.
Hassainiyaani, na allamah ssayyid Murtadhwa al-isfahaiy na allamh ssayyid Ahmad Al-madadi, na allamah shekh baaqir Iirawaniy,na wengine ambao ni walimu wakubwa na wenye fadhila wa hawza ya kielimu.
Pamoja na mheshimiwa sayyid, kujishuhulisha na usomaji na kufanya utafiti (Bahth) katika muda huu pia sayyid (mungu amlinde) alikuwa amelitilia umuhimu sana, suala la uandishi wa vitabu muhimu na risalatul-amaliya ili kuiongezea au kuijaza maktaba ya kielimu ya dini kwa vitabu vingi vilivyo madhubuti na vizuri, ukiongezea vitabu vya masomo vya walimu alivyo viandika kama vitabu vya fiqhi na usul.
Na ifuatavyo ni orodha ya majina ya baadhi ya vitabu vyake.